Chama Cha Mapinduzi wa Iringa kwa kushirikiana na Mawakili wa TLS pamoja na Wanasheria toka Jumuiya ya Wanawake Taifa kufuatia Tamko la Mwenyekiti Merry Chatanda kuhusu kesi ya mama Maria Ngonda aliyehukumiwa miaka 22 kisa nyama ya swala jopo hilo lilifika gerezani na kuzungumza na mama huyo ili kuona namna gani ya kumsaidia.Tiari jopo la wanasheria wanawake wameshafika mkoani Iringa kwaajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo upya na tiari wameshaonana na mama Maria Ngoda na kuongea na mawakili pamoja na wanasheria
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake mkoa wa Iringa Zainabu Mwamwindi amesema wanaimani mwanamke mwenzao atapatiwa haki yake
Ikumbukwe mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa ilimuhukumu kifungo cha miaka 22 jela Maria Ngonda mkazi wa mtaa wa zizi la n’gombe iliyopo manispaa ya Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.