Mawakili wa Sean “Diddy” Combs walidai katika mahakama madai yaliyowasilishwa Jumanne kwamba video zinazoonyesha matukio ya ngono ya rapa huyo, mpenzi wake wa zamani Cassie Ventura na vijana wakiume “zinathibitisha kutokuwa na hatia kwa Bw. Combs” kwa sababu zinaonyesha ngono kati ya “watu wazima waliokubali na sio kulazimishwa.”
Kuna video tisa ambazo waendesha mashitaka wamedai Combs aliziita “freak offs” zilizoelezewa na waendesha mashitaka kama “maonyesho ya kina ya ngono” ambayo kwa sasa yanapatikana kwa mawakili wa utetezi kutazama.
“Kinyume na kile ambacho serikali imesababisha Mahakama hii na umma kuamini, kile kinachojulikana kama ‘Freak Offs’ zilikuwa ni ngono za kibinafsi kati ya watu wazima wenye ridhaa kamili wenye uhusiano wa muda mrefu,” mawakili wa utetezi Marc Agnifilo na Teny Geragos walisema.