Tume huru ya Taifa ya uchaguzi imewataka mawakala wa vyama vya siasa kutoingilia majukumu ya watendaji wa daftari la Kudumu la wapigakura wakati wa utekelezaji wa zoezi la uboreshaji wa taarifa za wapigakura kwenye vituo vya uandikishaji.
Rai hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Jaji Mstaafu wa Mahakama ya rufani Mbarouk Salim Mbarouk leo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo Kwa watendaji ngazi ya mkoa kuhusu uboreshaji wa daftari la Kudumu la wapigakura mkoani Tanga.
Amewataka mawakala wa vyama vya siasa kuwasaidia watendaji kutambua waombaji wa eneo husika na hivyo kusaidia kuongeza uwajibikaji na uwazi wakati wa zoezi la uboresho wa daftari hilo.
“Mawakala wa vyama vya siasa wakati wa uboreshaji wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kujiandikisha Ili kuleta uwazi wa zoezi Zima lakini na kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizo kuwa za lazima”alisema Jaji Mbarouk.