Vijana wa Tanzania wametakiwa kujiamini na kutokata tamaa katika kutafuta na waamini wanachokifanya kama wanataka kusonga mbele katika kutimiza malengo yao kwa kuongeza kipato binafsi na kutengeneza fursa za ajira.
Imekuwa mara chache sana kwa vijana wa kitanzania kuanzisha kampuni zao binafsi ambazo huzisimamia na kuziongoza wenyewe baada ya kuhitimu masomo yao na badala yake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa ajira.
Ayo TV na millardayo.com leo May 2, 2017 imepiga stori na mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya Maxcom Africa, ambayo ni kampuni ya Tanzania inayomilikiwa na watanzania Eng. Juma Rajabu ambapo moja kati ya mambo aliyotolea ufafanuzi ni namna walivyoanzisha kampuni hiyo na mipango wanayokuja nayo mwaka huu.
Aidha, kampuni hiyo imetambulisha Bodi ya Wakurugenzi ambayo itakaa kwa miaka mitano ijayo hadi mwaka 2022 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Samuel Wangwe na wataalam wengine.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Sababu zilizotajwa kumsamehe Halima Mdee baada ya kumtukana Spika. Bonyeza play kutazama…