Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro amempa siku tatu kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutoa taarifa sahihi ya michango ya rambirambi zilizotolewa kwa familia za watu 36 waliofariki katika ajali iliyotokea Karatu Arusha.
Meya Kalist amesema >>>Kumekuwa na maneno mengi hapa Arusha kuhusu pesa za rambirambi, watu wamekuwa wakinipigia simu na kuuliza lakini kwavile hakuna mtu yeyote aliyehusika kukusanya na kutumia michango zaidi ya Mkuu wa Mkoa namtaka atoe ufafanuzi wa fedha zilizochangwa.
Nampa siku ya leo na kesho asipokuja hadharani kuwaeleza wananchi nama fedha zilivyotumika nitaweka hesabu niliyonayo mimi hadharani kwasababu wananchi waliopeleka hela kwa Mkuu wa Mkoa ni wa Arusha<<<- Meya Kalist Lazaro
Kufahamu kila kitu alichosema Meya Kalist Lazaro bonyeza p.y hapa chini kutazama.
VIDEO: Ulikosa kutazama video ya wanafunzi walionusurika kwenye ajali Arusha wakipelekwa Marekani kwa ndege? Tazama hapa