Habari za Mastaa

Eti itawezekana Floyd Mayweather amkimbie Manny Pacquiao ??

on

city

Floyd Mayweather ana jukumu la kuuthibitishia ulimwengu kwamba yeye bado ni mbabe ambaye hataki kupoteza pambano lolote kwenye ulingo.. Manny Pacquiao nae ana jukumu la kukaza msuli ili ahakikishe anatengua rekodi ya Mayweather.. watu wanahesabu saa kadhaa tu historia iandikwe pale MGM Grand Garden ArenaLas Vegas Marekani.

Siku moja tu kabla ya pambano hilo kufanyika, kocha wa Pacquiao, Freddie Roach ametamka kuwa huenda Maywether akagoma kupanda ulingoni siku ya pambano hilo kwa kuwa anahisi Floyd hakutaka pambano hilo liwepo ila wamamlazimisha.

floo

pac

Mabondia hao usiku wa jana walikutana na waandishi wa habari na kuonyesha mkanda ambao mshindi atakabidhiwa baada ya mchezo huo.

etiii

Kwa pamoja wamekutana na kila mtu ametoa ya moyoni, lakini kila mmoja kajigamba kushinda pambano hilo.. tusubiri tu hiyo kesho usiku kutakuwa na majibu gani ambayo dunia itayapata kutoka kwenye pambano.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments