Leo May 1, 2017 Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zimefanyika katika Viwanja vya Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam, sherehe za maadhimisho hayo zimefanyiaka kwenye uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wafanyakazi ‘TUCTA’.
Akizungumza kwenye sherehe hizo, Margaret Sitta amewasisitiza waandaaji kuwa sio lazima kutegemea Waziri kuwa mgeni rasmi bali wao wenyewe wanaweza kuwa na kujadili mambo yao.
Bonyeza play kutazama…
VIDEO: Agizo la Rais Magufuli alilolitoa leo mkoani Kilimanjaro, Bonyeza play hapa chini kutazama