Israel na Hamas wataanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kuhusu hatua ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano wiki hii, maafisa wamesema.
Mazungumzo yalipaswa kuanza tarehe 4 Februari, lakini wapatanishi walisema mazungumzo hayo hayajaanza.
“Itatokea wiki hii,” waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar aliambia mkutano wa wanahabari mjini Jerusalem jana.
Awamu ya pili ni ipi?
Ikikubaliwa, inatarajiwa kujumuisha kuachiliwa kwa mateka wote waliosalia, wakiwemo wanajeshi wa kiume wa Israeli, usitishaji wa kudumu wa mapigano na uondoaji kamili wa vikosi vya Israeli.
Israel inasema haitakubali kujiondoa kabisa hadi uwezo wa kijeshi na kisiasa wa Hamas utakapoondolewa, kuhakikisha haiwezi kutawala tena, huku Hamas ikikataa kuwakabidhi mateka wa mwisho wa Israel hadi Israel itakapomaliza vita na kuwaondoa wanajeshi wake wote.