AyoTV

“Katikati yetu wametokea watu wakatili”-Waziri Nchemba (+Video)

on

January 2, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba amezungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Dodoma na kuelezea mpango mkakati wa Wizara yake katika kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha mwaka mpya wa 2018.
 Waziri Nchemba amesema…>>>“Mwaka 2018 kaulimbiu yetu ni zuia uhalifu kabla haujatokea, sisi kama Serikali na Wizara jukumu letu ni kuzuzia uhalifu kabla haujatokea. Watu waache mazoea ya amani tuliyokuwa tumeishiba sana, katikati yetu wameshaanza kutokea watu wenye mioyo ya kikatili na kinyama ambao wanauwezo wa kufanya vitu vya kinyama zaidi

“Kila mmoja wetu hivi sasa awe na wivu, awe na uzalendo kwa nchi yake aone kwamba mhalifu anapataje nafasi ya kupita katika nchi yetu kwamaana hiyo mtanzania yeyote akiona mtu haelekei na mazingira atoe taarifa ili tuwe mbele na tukio” –Waziri Nchemba

Uamuzi wa TCRA kwa vyombo vya habari vilivyokiuka kanuni za Utangazaji

Soma na hizi

Tupia Comments