Top Stories

Kauli ya kwanza ya Mwigulu tangu atenguliwe “Nitaacha Ubunge?”

on

Ikiwa zimepita takribani siku sita tangu Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri ikiwemo kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba na nafasi hiyo kuchukuliwa na Kangi Lugola.

Leo July 7, 2018 Dr Nchemba kwa mara ya kwanza tangu kutenguliwa kwake amefanya mkutano na wananchi wake wa jimbo la Iramba Maghairi na kuzungumza nao ikiwemo tetesi za mitandaoni kwamba anataka kujiuzulu nafasi ya Ubunge baada tu ya kutenguliwa katika nafasi ya Uwaziri.

Nimesikiasikia kwenye mitandao kwamba Ooooh! Nitaacha na Ubunge, uliona wapi mchezaji asajiliwe kwenye club yake ya kuchezea akaonekana team ya taifa alafu siku akiondoka team ya taifa aseme hata club yenu sichezei. Hili sio jambo la ugomvi na wala msipate shida. Nilipopata fursa ile kuna mambo mlikuwa mnakosa kwasababu muda mwingi nilikuwa na majukumu ya kitaifa” –Dr Mwigulu Nchemba

Soma na hizi

Tupia Comments