Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Sweden amebainisha siku ya Jumanne Oktoba 15, 2024 kwamba inafanya uchunguzi kuhusu ubakaji baada ya ziara ya Kylian Mbappé na wasaidizi wake wiki iliyopita huko Stockholm, bila hata hivyo kutaja majina yoyote, huku vyombo vya habari vya Sweden vikithibitisha kwamba nyota huyo ndiye kiini cha uchunguzi.
Gazeti moja liliripoti kwamba polisi wa Uswidi wanachunguza tukio linalodaiwa kuwa la ubakaji katika Hoteli mahali ambapo Mbappe na wasaidizi wake walikuwa wamelala usiku mmoja.
Wakati huohuo, msafara wa Mbappe wamekashifu ripoti hii, wakidai kuwa hilo lilikuwa ni jaribio la kumharibia mwanasoka huyo jina na sifa, kabla ya kusikilizwa kwa mishahara isiyolipwa.
Wakati huohuo, timu ya Mbappe pia imedai kuwa hatua zote za kisheria zitachukuliwa kurekebisha hadhi ya fowadi huyo wa Ufaransa na kurejesha ukweli ikiwa ni lazima.
Zaidi ya hayo, timu hiyo pia ilidai vikali kwamba tuhuma dhidi yake ni ‘za uwongo na kutowajibika’, kulingana na ripoti ya The Sun