Michezo

Mbappe hawatoa hofu PSG haondoki

on

Staa wa club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Kyliane Mbappe amethibitisha kuwa ataendelea kuwa katika club hiyo kwa msimu ujao tena licha ya kuwa amekuwa akihusishwa kuwa katika rada za Real Madrid kwa muda mrefu na sasa Mabingwa hao wa Hispania wanadaiwa kuongeza nia.

“Bado niko hapa niko katika mradi wa miaka minne ijayo kutimiza miaka 50 kwa hii club ni muhimu sana kwa club, mashabiki na kila mmoja, hivyo nitakuwa pale haijalishi itakuwaje, nitajaribu kuleta mataji kwa kushirikiana na wenzangu na nitajitoa sana kwa ajili ya club”>>> Mbappe

Mbappe ambaye ni moja kati ya wachezaji muhimu katika club ya PSG alijiunga na club hiyo 2015 akitokea AS Monaco ambayo alionesha uwezo mkubwa katika kucheza soka kiasi cha kuvivutia vilabu mbalimbali barani Ulaya wakati ambao alikuwa na umri wa miaka 16.

VIDEO: KIMENUKA YANGA, MORISSON KASUSA AKIMBIA NJE UWANJANI “ACHA MASHABIKI WANIPIGE”

Soma na hizi

Tupia Comments