Kylian Mbappe huenda asiwe na kikosi cha Real Madrid kwa ajili ya kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Mabingwa hao wa Uhispania na Ulaya wanatarajiwa kusafiri kwenda Marekani Julai 28 na watacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Milan (Chicago), Barcelona (New Jersey) na Chelsea (Charlotte).
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Madrid kwa uhamisho wa bure kutoka Paris Saint-Germain msimu huu wa joto na alitambulishwa kwa mashabiki wa klabu hiyo Jumanne.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Mbappe aliulizwa kuhusu uwepo wake kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya na alijibu: “Kama klabu inataka niende, nitakwenda.”
Klabu hiyo imechukua uamuzi kwamba hatakwenda, na badala yake ataanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya na wachezaji wenzake wapya wa klabu hiyo kwenye vituo vyao vya Valdebebas kuanzia Agosti 7.
Mpango wa klabu hiyo uliochukuliwa kwa kushirikiana na Mbappe ni mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kucheza katika michuano ya Kombe la Super Cup dhidi ya Atalanta Agosti 14 mjini Warsaw, Poland.
Madrid pia ina mpango wa wachezaji wenzake wa kimataifa wa Mbappe Ferland Mendy, Aurelien Tchouameni na Eduardo Camavinga kurejea mazoezini wakati huo huo na Mbappe, ingawa inaweza kubadilika kulingana na matakwa ya wachezaji.
Baada ya kutolewa kwenye michuano ya Euro 2024 na Uhispania kwenye hatua ya nusu fainali Julai 9 na kuwasilishwa Santiago Bernabeu Julai 16, klabu hiyo, Carlo Ancelotti na Mbappe mwenyewe wameona ni vyema apumzike kimwili na kiakili kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. kuanza maisha katika klabu yake mpya.