Habari za Mastaa

Maneno ya Mbasha kuhusu Mume mpya wa Flora na aliyevunja ndoa

on

Muimbaji wa muziki wa Injili Emmanuel Mbasha ambaye pia alikuwa Mume wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Florance Henry ‘Madame Flora’ kwa mara ya kwanza amezungumzia Mwanaume aliyemuoa Flora anaeitwa Daudi Kusekwa.

Ilikua ni kwenye TV show ya SHILAWADU usiku wa May 5, 2017 Mbasha amesema kuwa hana tatizo na David Kusekwa ambaye ndiye mume wa Madame Flora bali tatizo lake liko kwa aliyesababisha ndoa yake kuvunjika.

“Sina tatizo naye ila yule aliyesababisha ndoa yangu kuvunjika huyo ndio mbaya wangu, Daudi sina ugomvi naye wowote… hajawahi kuniingilia kwenye mahusiano yangu nikiwa katika ndoa, hajawahi kunivurugia mipango yoyote’

‘Simfahamu Daudi na ninaamini pia na yeye alikuwa hanifahamu labda kama alikuwa ananijua kama Mbasha kwa kuwa nilikuwa najulikana.” Emmanuel Mbasha.

Kauli hiyo ya Mbasha imekuja wakati akijibu swali kuwa anajisikiaje Mtoto wake kumuita David Kusekwa baba:

“David alikuwa hajui kama kuna siku atakuwa na Flora kwahiyo sina la kumchukia na hakuwahi kuniingilia hata mwanangu akimuita baba  siyo tatizo japo sijui atamuitaje, kama atamuita baba mdogo haina tatizo, naamini atakuwa mtu mwema, sidhani kama atamfanyia kitu kibaya mwanangu.”

Pamoja na hayo Mbasha ametoa ushauri kwa mume huyo mpya wa Madam Flora akisema anamtakia maisha mema akidai anamkubali kwa sababu hakuwahi kumuingilia katika mahusiano yake.

“Namkubali ni mtu ambaye hajawahi kuniingilia kwenye mahusiano yangu au katika ndoa yangu so ni mtu flani tu naweza kumuita mstaarabu, wamekutana, wakakubaliana kuoana wakati ambao mimi na Flora tuliachana kisheria, mimi sina tatizo na jamaa kwa hiyo awe na amani ya kutosha waendelee na maisha.” 

EXCLUSIVE VIDEO: Florah kuhusu kumualika harusini mume wa zamani na kumzidi umri mume mpya

EXCLUSIVE VIDEO: Mume mpya wa Flora afunguka baada ya ndoa, tazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments