Habari za Mastaa

Menina aonekana BASATA, alichojieleza mbele ya Viongozi

on

Msanii Menina Abdulkarim ambaye anafanya kazi zake za sanaa kama Msanii wa Bongo flava, MC, na Muigizaji wa filamu amefika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA) zilizopo Sharif Shamba,Ilala jijini Dar Es Salaam ili kutoa maelezo yake juu ya kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii.

Kupitia mahojiano kati ya Msanii na BASATA kwa pamoja wamesikiliza maelezo ya Msanii Menina Abdulkarim na nini kilichojitokeza katika sakata zima la kusambaa kwa video na picha zake za utupu kupitia mitandao ya kijamii. Kwa kuwa suala la kusambaa video na picha za utupu za Msanii Menina katika mitandao ya kijamii lipo mikononi mwa mamlaka nyingine,BASATA imeamua kuyafanyia kazi maelezo yake.

Mara kadhaa BASATA kupitia utaratibu wake wa kutoa Elimu kwa wasanii na Umma wamekuwa wakiwaelekeza wasanii wote kote nchini kufanya kazi zao za Sanaa kwa kuzingatika maadali mema kwa jamii,pamoja na kufuata taratibu za kujisajili,lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wasanii wamekuwa hawazingatii maelekezo hayo na hivyo kujikuta wanavunja sheria za nchi.

WALIMU NA WANAFUNZI WAFUNGUKA MOTO ULIVYOTEKETEZA BWENI LOTE NA VIFAA

Soma na hizi

Tupia Comments