Michezo

Mbeya City wamfukuza kazi kocha Amri Said

on

Club ya Mbeya City ya Mbeya mara baada ta kupoteza mchezo wake wa leo 2-1 dhidi ya Mwadui FC mkoani Shinyanga imemfuta kazi rasmi kocha wao Mkuu Amri Said.

Mbeya City hadi wanafikia uamuzi huo usiku huu wapo nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2020/21 wakiwa na point 2 na hawajawahi kushinda katika mechi zao zote 7 walizocheza.

Hata hivyo Mbeya City wamechukua tahadhari mapema baada ya msimh uliopita kunusuruka kushuka daraja, hivyo uingozi chini ya mtendaji wao mkuu Mr Kimbe wameamua kuchukua tahadhari mapema.

Soma na hizi

Tupia Comments