Michezo

Mbeya City yampa mkono wa kwa heri Juma Mwambusi

on

Moja kati ya makocha wenye heshima kubwa katika club ya Mbeya City ya jijini Mbeya ni pamoja na kocha Juma Mambusi ambaye anapewa heshima kubwa katika ckub hiyo kutokana na kuwahi kuifundisha timu hiyo na kuwa tishio kwa vigogo Tanzania.

Mbeya City leo imetangaza kuachana na kocha huyo baada ya kuomba mwenyewe ajiuzulu kwa sababu ya timu yake kutofanya vizuri, Mwambusi akidaiwa kuandika barua ya kujiuzulu November 26 na November 30 ndio imekubaliwa.

Juma Mwambusi anaondoka timu hiyo ikiwa nafasi ya 19 katika Ligi Kuu kwa kubaki na point 8 na imecheza michezo 12.

Soma na hizi

Tupia Comments