Ni Afisa Tarafa Sindeni ndg, Sijaona Bugufi ambapo amefanya kikao cha Utatuzi wa Kero za Wananchi zinazowakabili Wananchi wa Kijiji cha Msomera wageni walihamia kwahiyali kupisha uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro na wenyeji waliopo kijiji cha Msomera.
Afisa huyo aliongozaana na wakuu wa Idara ya Halmashauri ya wilaya na Wakuu wa Taasisi zote Tarura, Tanesco, Ruwasa na NCAA
Kikao hicho kimefanywa baada ya maelekezo ya Mh Mkuu wa Wilaya ya Handeni kuhakikisha wananchi hao wanaishi kwa amani na utulivu.
Wananchi wameishukuru Serikali kwa hatua hiyo ya utatuzi wa changamoto ambapo changamoto kubwa ilikua ya ugawaji wa mashamba kwa wageni bila kuwapatia wenyeji kamaa alivyoelekeza Waziri Mkuu. Ambapo wageni nao watapatiwa mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 zoezi linaenda kuanza mapema mwezi January mwishoni.