Top Stories

Viongozi wa Dini wanamfungukia JPM “Baba Demokrasia, waache ‘wapinzani’ waongee” (+video)

on

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Amani Lyimo amemuomba Rais Magufuli kuwaachia uhuru wananchi wazungumzie inapowezekana kwa sababu hiyo ndiyo Demokrasia.

Mchungaji Lyimo amesema “Tunakuomba Baba unafanya kazi sana lakini Baba Demokrasia, Watanzania wengi wana hofu, wengi hawadhubutu kuzungumza wana hofu nakuomba Rais kama kuna uwezekano Baba waachie pumzi wazungumze lakini hawata kushinda” 

“Rais unafanya kazi nzuri sana, lakini naomba uwaachie pumzi kidogo nao waongee maana hata wewe unafanya kazi nzuri hawatakushinda, watu wanachagua kazi na si maneno kwa maana kazi zinanoonekana” Mch. Amani Lyimo, Mchungaji wa kanisa la KKKT

“Zamani wakati dhehebu jipya linataka kuanzishwa ilikuwa Baraza la Dini husika linakaa kisha linatoa mapendekezo ndipo dhehebu hilo linaruhusiwa, lakini siku hizi kila kukicha Makanisa yanaanzishwa kama vile injili imekuwa biashara” Mchungaji wa Kanisa la KKKT

Lulu kaibuka na mapya “Nimeamua kuuza nguo zangu nipate pesa”

Soma na hizi

Tupia Comments