Jukwaa linaloratibu mbio za Wanawake nchini linalofahamika kama Tanzania Women’s Run limeandaa msimu wa tatu wa mbio hizo zinazohusisha ushiriki wa mbio za wanawake zitakazofanyika katika Viwanja vya Coco Beach jijini Dar Es Salaam zikiwa na kauli mbiu ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Mratibu wa Mbio hizo Pili Amiri Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa mbali na mbio hizo pia litafanyika zoezi la ukusanyaji wa taulo za kike kwa mabinti wenye mahitaji maalum kupitia wadau mbalimbali na sehemu ya mapato yatokanayo na mbio hizo ambapo Mshiriki atatakiwa kulipa kiasi cha Tsh 35,000/=.
Mbali na hivyo mbio hizo zimelenga pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi kwa Wanawake, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya pamoja na uchumi, ukatili dhidi ya watoto na mengineyo.