Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Rais wa Shirika la Meli la COSCO kutoka nchini China, Bw. YangFan Chen kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya TPA na COSCO.
Katika mazungumzo yao Viongozi hao wamejadili namna bora ya kushirikiana ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za shehena zinazoingia na kutoka nchini.
Bw. Chen ambaye alifuatana na Watendaji waandamizi wa kampuni hiyo pamoja na kampuni tanzu ya SINOTASHIP, wametembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma
Bandarini, ameahidi kuendeleza ushirikiano na TPA ili Wateja wao waendelee kupata huduma bora na ya haraka.