Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Mbosso na Boss wa Samsung mkutano wa wadau
Share
Notification Show More
Latest News
Video: Rais Samia amuibua Ally Hapi, Afunguka haya
March 22, 2023
Mfungo wa Ramadhan Kaya 1000 zapatiwa vyakula “Tunarudisha kwa Jamii”
March 22, 2023
Jamaa aangusha gari Mtaroni, Dereva haonekani, mashuhuda wasimulia, ‘Alikuwa anaongea na simu’
March 22, 2023
Wanywaji Pombe wapewa alama tatu, “mdogomdogo, Wajawazito na Madereva”
March 22, 2023
“Serikali kutenga Fedha kulinda hadhi ya urithi wa Mji mkongwe Zanzibar”- Rais Mwinyi
March 22, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Habari za Mastaa > Mbosso na Boss wa Samsung mkutano wa wadau
Habari za Mastaa

Mbosso na Boss wa Samsung mkutano wa wadau

March 16, 2022
Share
4 Min Read
SHARE

Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na wadau wake wa kibiashara katika hoteli ya Hayatt Jijini Dar es Salaam wakiwemo wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake zote kutoka pande zote za nchi ya Tanzania.
 Mkutano huo umeandaliwa na Bw. Tae Sun Lee, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki.

Lengo kuu la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wakuu wa bidhaa za Samsung wakiwemo wasambazaji na wafanyabishara ili kuhakikisha matumizi bora zaidi yanatolewa kwa mtumiaji wa bidhaa za Samsung.
Kampuni ya Samsung inaendelea kuamini kuwa maendeleo ya kiteknolojia ndio kichocheo kikuu cha biashara ya bidhaa zake ulimwenguni.

Katika mkutano huo, bidhaa mbalimbali za Kampuni ya Samsung za mwaka 2022 zimeonyeshwa zikiwemo simu ambapo bidhaa hizo zikilenga kikazi cha millennia, Z.
Akiongea wakati akiwasilisha mada katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Bw. Lee amesema kuwa Kampuni ya Samsung itaendelea kuimalisha mahusiano yao na washirika wao wakiwemo wasambazaji wote kutoka pande zote za Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Msanii wa muziki Mbosso akiwa na Mabosi wa Samsung Afrika katika mkutano wa wadau wa mawasiliano na wafanyabiashara .

Bwana Lee amesema kuwa Kampuni ya Samsung itaendelea kuhakikisha bidhaa zote zinazotengenezwa na Kampuni hiyo zinaendelea kuwa zenye ubora wa hali ya juu ili kumpa furaha na faraja mtumiaji wake.

Ameongezea kuwa mkakati mkubwa wa Kampuni ya Samsung ni kuendelea kuona bidhaa zake za kielektroniki zinaendelea kuwa bidhaa pendwa kabisa katika soko la Afrika.

Katika mkutano huo, Millicom Tanzania PLC [Tigo] wameweza kuanzisha mashirikiano na Kampuni ya Kieleckroniki ya Samsung ikiwa ni mpango kabambe wa kumuwezesha mteja anayetumia Samsung ‘Smart TV’ kuweza kupata kifaa cha kumuwezesha kutumia intanet kwenye luninga yake cha Mi-Fi kutoka Tigo.

Katika makubaliano hayo, mteja atakaye atanunua luninga ya Samsung smart katika kipindi cha ofa ataweza kupata kifaa hicho cha MiFi kutoka Kampuni yaTigo kikiwa na kifurushi cha kuanzia ili kumuwezesha kujiunga na mtandao wa intanet katika luninga yake

Naye, Afisa Mkuu (Mikakati na Ubunifu) wa Kampuni ya Tigo David Umoh amesema: “Kama Tigo, kupitia teknolojia tunalenga kufanya maisha ya Mtanzania kuwa bora zaidi ndiyo maana tumeamua kushirikiana na Kampuni ya Samsung katika kuhakikisha kila mteja atakaye nunua Smart TV ya Samsung anapata kifaa cha intanet cha MiFi kutoka Tigo.”

Bwana Umoh ameongezea kuwa kampuni ya Samsung imekuwa mmoja wa washirika wao wakuu nchini Tanzania na amesisitiza kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja ikiwa ni katika mipango chanya ya kuhakikisha maisha ya Mtanzania yanakuwa bora zaidi.

Zaidi ya hayo, Kampuni ya kielectroniki ya Samsung iliunganisha pamoja kitengo chake cha simu pamoja na kile cha watumiaji wa bidhaa mbali mbali kuwa kitengo kimoja cha DX.

Lengo kuu la kuweza kuwa na kitengo kimoja ni kumuwezesha mtumiaji wa bidhaa za Samsung kupata huduma zote sehemu moja.

Kampuni ya Samsung imetanabahisha kuwa wataendelea kutengeneza bidhaa mbalimbali na kutoa huduma bora zaidi ili kuendela kudumisha mahusiano yao na watumiaji.

“Kama Samsung tunasisitiza kuwa tutaendelea kuwa na sauti moja pale tunapoweka mikakati yetu ili tuweze kwenda mbele. Mienendo yetu ya soko inaendelea kubadilika na pia tunaona haja ya kurekebisha katika maeneo mbali mbali ili kukidhi mahitaji ya wadau,” Bw. Tae Sun Lee, Mkurugenzi Mkuu, Samsung Electronics Afrika Mashariki alisema.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kampuni ya Samsung ulihudhuriwa na wadau mbali mbali wa Kampuni hiyo wakiwemo wafanyabiashara zaidi ya 100 waliokutana na kujadili mahitaji ya soko na jinsi gani kwa pamoja wanaweza kukuza soko la Samsung nchini Tanzania.

You Might Also Like

Sina Tatizo na yeye, mteule wa Rais hanuniwi” Steve Nyerere Kafunguka (+video)

Rihanna & Asap rocky waipanga ndoa yao ya siri , barbados hivi karibuni

MTOTO WA BECKHAM APOST SAA YA MIL 97, ANYWA POMBE NA BABA YAKE

MADONNA AWAJIBU MASHABIKI MUONEKANO WAKE MPYA BAADA YA UPASUAJI!

PROFILE: Mfahamu Vido Vidox, ripota wa Ayo TV kwa stori za mastaa!!

TAGGED: habari za mastaa
Pascal Mwakyoma TZA March 16, 2022
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 16, 2022
Next Article TBS yatoa wito wasafirishaji bidhaa nje ya nchi kupima kabla ya kuzisafirisha
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Video: Rais Samia amuibua Ally Hapi, Afunguka haya
Top Stories March 22, 2023
Mfungo wa Ramadhan Kaya 1000 zapatiwa vyakula “Tunarudisha kwa Jamii”
Top Stories March 22, 2023
Jamaa aangusha gari Mtaroni, Dereva haonekani, mashuhuda wasimulia, ‘Alikuwa anaongea na simu’
Top Stories March 22, 2023
Wanywaji Pombe wapewa alama tatu, “mdogomdogo, Wajawazito na Madereva”
Top Stories March 22, 2023

You Might also Like

Top Stories

Video: Rais Samia amuibua Ally Hapi, Afunguka haya

March 22, 2023
Top Stories

Mfungo wa Ramadhan Kaya 1000 zapatiwa vyakula “Tunarudisha kwa Jamii”

March 22, 2023
Top Stories

Jamaa aangusha gari Mtaroni, Dereva haonekani, mashuhuda wasimulia, ‘Alikuwa anaongea na simu’

March 22, 2023
Top Stories

“Serikali kutenga Fedha kulinda hadhi ya urithi wa Mji mkongwe Zanzibar”- Rais Mwinyi

March 22, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?