Ni Machi, 18, 2022 ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe anazungumza na vyombo vya habari muda huu.
“Nimekua gerezani kwa muda mrefu lakini nimejifunza sana. Niwahakikishe watanzania na dunia yote kwamba sikupoteza zile siku. Nimezitumia kujiimarisha kifikra, kimtazamo na hata moyo wangu umebadilika sana.”- Mbowe
“Nawaomba wanaChadema wenzangu tusiwe na chuki na yeyote katika mapambano haya kwa sababu mapambano haya ni kupigania uhai wa watu, ni kupigania ustawi wa watu. Kamwe hatuwezi kutafuta ustawi wa watu wakati tunatafuta visasi. Visasi sio utamaduni wa chadema,sio utamaduni wa Mbowe“- Mbowe
“Nililetewa salamu za mheshimiwa Rais kwamba angependa kukutana na mimi mapema iwezekanavyo.Mtakumbuka kwa muda mrefu sisi kama chama tulitaka kuzungumza na Rais tukiamini kwamba ana majibu ama ana ufunguzi wa mambo mengi yanayolisibu taifa”- Mbowe
Kwa bahati mbaya hatukupata nafasi ya kukutana nae hadi ninakwenda gerezani. Kwa hiyo nikiwa gerezani siku natoka nikaambiwa kwamba mheshimiwa Rais angependa kukuona haraka. Nimetoka gerezani kwa moyo mweupe, wala sikutoka na kiburi, cha kwamba naweza nikapuuza mualiko wa Rais’- Mbowe
LIVE: MBOWE ANAONGEA “NIMETOKA GEREZANI KWA MOYO MWEUPE, KATIBA NI AJENDA YETU, SISI SIO MAGAIDI”
HARMONIZE AFIKA CHATO, ASHIRIKI KUMBUKIZI YA HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI