Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimezindua mfumo wake mpya wa Kidigitali wa uendeshaji wa Chama hicho ambapo kitakuwa kikikusanya ada za Unachama wa wanachama wake na kukifanya kujitegemea.
Mbowe amesema “Leo tunazindua mfumo wa Kidigitali tutahama kutoka Analog tutahamia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji, tunahitaji kujenga chama kitakachojitegemea, kwa sababu Serikali inafikiri chama hichi kinategemea sana Ruzuku“.