Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akizungumza kwenye Baraza Kuu la Chama hicho ameweka wazi alichomwambia Rais Samia Ikulu Dar es Salaam.
“Nilipotoka gerezani nilipata mwaliko wa kwenda Ikulu, nilisita kidogo lakini sikujitiakiburi nilikwenda kuonana na Rais na sio Rais Samia pekee yake hata angekuwa IGP Sirro ningekwenda kumuona, wajibu wangu kama Kiongozi ni kuweka pride zangu chini kwenda kusimamia maslahi ya Chama chetu”- Mbowe
“Nilimwambia Rais Samia Taifa letu lina tatizo kubwa na linatuhitaji wote tunapaswa kuzungumza kutafakari ni nini kinachotenga Taifa letu, nilimwambia Rais kuna kuna mambo mengi ambayo kama Taifa yanatutenga kwasababu mliopo madarakani mmekubali Taifa letu kutengeneza matabaka”- Mbowe
“Nikamwambia Madam President mmekuwa mkihubiri amani, amani huku mkisahau msingi mkuu wa amani nao ni haki, nikamwabia nimechoka kuona Viongozi wangu wakipelekwa gerezani, sio sifa kuona Vijana wa CHADEMA wanapigwa risasi, nilimwambia Rais Samia kuwa tujenge misingi ya kuaminiana, niliamini katika kukutana ili kuliponya Taifa na kama njia ya kumaliza tofauti zetu”- Mbowe
“Ziara yangu kwenda kwa Rais Samia inaonekana ni jambo la miujiza, na inaonekana hivyo kwasababu tumejenga utamaduni wa kutoaminiana, akionekana Mpinzani Manakwenda Ikulu inaonekana pengine hapa pana biashara”- Mbowe