Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, amechaguliwa kuongoza kiti cha Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kupata ushindi wa kishindo kwa kupigiwa kura 886 na kumburuza mgombea mwenzake, Cecil Mwambe aliyepata kura 56 pekee.
Matokeo ya Uchaguzi huo yametangazwa leo na Msimamizi wa Uchaguzi huo Sylvester Masinde, kufuatia uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo.
“Bwana Cecil Mwambe amepata Kura 59 sawa na asilimia 6.2, Freeman Aikael Mbowe amepata kura 886, sawa na asilimia 93.5, Kura zilizoharibika ni tatu kwa matokeo haya napenda kumtangaza Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wetu wa chama wa awamu inayokuja” Sylvester Masinde.
Aidha katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara, imechukuliwa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, ikichukuliwa na Said Issa Mohammed.
MPINZANI WA LISSU: ”MIMI NI FUNDI WA CHENGA, LISSU KAFUNGA MAGOLI”