Top Stories

Mbowe na wenzake kujitetea Machi 4, 2022

on

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake wanatarajia kuanza kujitetea Machi 4, 2022 baada ya kukutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu.

Baada ya Mbowe na wenzake kukutwa na kesi ya kujibu mbele ya Jaji Joachim Tiganga, waliondolewa katika mahakama hiyo na kurejeshwa gerezani.

Mbowe na wenzake watatu wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 5 kati ya 6.

Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya.

MBOWE AKIONDOKA KWENDA GEREZANI WAFUASI WA CHADEMA WAPIGA SHANGWE BAADA YA KUMUONA

Soma na hizi

Tupia Comments