Top Stories

Mbowe na wenzake wana kesi ya kujibu Mahakamani

on

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu imemkuta na kesi ya kujibu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika mashitaka 5 kati ya 6 hivyo wanapaswa kuanza kujitetea.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Joachim Tiganga ambapo amesema Mahakama imepitia ushahidi wote wa Jamhuri wa Mashahidi 13 ambao umewafanya Washitakiwa wakutwe na kesi ya kujibu.

Hata hivyo Mahakama hiyo imemuachia huru Mshtakiwa wa kwanza baada ya kutokuwa na kesi ya kujibu katika shitaka la sita la kukutwa na sare na vifaa vya Jeshi licha ya kwamba atajitetea katika makosa mengine.

“Katika shitaka la 6 linalomkabili Mshtakiwa wa kwanza…. hajakutwa na kesi ya kujibu, hivyo katika kosa hilo yupo huru” ——— Jaji

KILICHOTOKEA MAHAKAMANI BAADA YA MBOWE KUKUTWA NA KESI YA KUJIBU

 

Soma na hizi

Tupia Comments