Mix

VIDEO: Mahakama kuu leo kwenye kesi ya Mbowe dhidi ya mkuu wa mkoa DSM na wenzake

on

Leo march 8 2017 mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam imeanza kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo “CHADEMA”, Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Kamishna  wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi kanda maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Leo Freeman Mbowe alifika mahakamani hapo lakini baada ya dakika kadhaa aliondoka mahakamani kabla ya kesi kusikilizwa na taarifa zinadai aliondoka ili kuhudhuria msiba wa mama wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, hata hivyo baadaye kesi iliendelea.

Nje ya mahakama hiyo wakili wa Freeman Mbowe, Hekima Mwasipu amezungumza na Ayo TV na millardayo.com na kusema kesi imetajwa na jaji ameamua hoja zitasikilizwa kwa njia ya maandishi na kesi itatajwa tena  March 30 2017.

VIDEO: Maamuzi ya mahakama kuu kuhusu ombi la Mbowe kutaka asikamatwe na Polisi, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments