AyoTV

“Viongozi lazima tujue kuna wakati wa kuwapisha wengine” –Dr Tulia (+Video)

on

January 14, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Joseph Magufuli katika  Misa Takatifu ya kusimikwa kwa Askofu wa  awamu ya nne wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya  Konde Dr Edward Johnson Mwaikali iliyofanyika katika Kanisa.

Katika salamu Dr Tulia alisema “Kwa namna ya kipekee kabisa kwa niaba ya Mheshimiwa Rais nitoe shukrani kwa namna mlivyomheshimu na kumpa fursa ili kama angeweza angekuwa mgeni rasmi lakini hata hivyo anashukuru kwasababu mngeweza kumualika mtu mwingine lakini mkampa yeye hiyo heshima.”

Leo nimejifunza jambo wakati nikiona Baba Askofu Mstaafu Dr. Israel Mwakyolile akikabidhi madaraka baada ya kuwa kwenye uongozi miaka kumi na sita, ni jambo jema kuondoka kwenye sehemu ukiwa bado watu kama wanakuhitaji… Madaraka yakitoka kwa mtu mmoja na kwenda kwa mtu mwingine kwa hali ya utulivu namna hii inatufunza hata sisi viongozi katika nafasi zetu lazima tujue kuna wakati wa kupisha wengine ili nguvu iongezeke zaidi na kasi iongezeke zaidi” –Dr Tulia

Alichoongea Kigwangalla baada ya kufanya ziara uwanja wa ndege na Dr. Mwigulu

Soma na hizi

Tupia Comments