Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe, Abdulaaziz M. Aboodamewataka Wenyeviti na Mabalozi Jimboni humo kufanya kazi kwa mshikamano ili kuboresha huduma kwa wananchi wanaowatumikia na kuweza kutimiza azma ya kuu ya Chama cha Mapinduzi ya kuwa na Umoja wenye nguvu kwa kuelendea kuwa Chama kisicho tetereka hapa nchi.
Mhe Abood ametoa wakati akifunga mafunzo maalum ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na Mabalozi wote wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Manispaa ya Morogoro, mafunzo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Tanzanite.
Mhe Abood ameweka wazi kuwa, Mabalozi ndio kiunganishi kikubwa baina ya wananchi na viongozi wa Serikali kwa maana ya kujua changamoto zao kabla ya kufikishwa kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na hivyo uhusiano bora kwa Viongozi hawa utaweza kuboresha kwa kiasi cha kuridhisha katika kuwatumikia wananchi waliowapa dhamana.
Aidha, Mhe Abood amebainisha kuwa, ushirikiano wa Wenyeviti na Mabalozi kwa miaka iliyopita imesaidia Ofisi yake kuweza kuhudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali zaidi ya Elfu 69,000 kwa hali hiyo kuendeleza usrikiano huo baina yao kutasaidia kuongeza idadi ya kuhudumiwa kwa wananchi kuanzia ngazi ya Shina, Mtaa, Kata hadi Wilaya na Jimbo kwa maana ya Ofisi ya Mbunge.
“Ushirikiano wenu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kufikiwa wananchi zaidi ya Elfu 69,000 kuhudumiwa kupitia Ofisi yangu kama Mbunge, hivyo changamoto zao zimeweza kutatuliwa kwa njia tofauti……. Niombe muendelee hivyo ili tuweze kuhudumia wananchi wengi zaidi”. Amebainisha
Katika hatua nyingine, amewaeleza Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi kuwa wanayo kila sabsabu ya kutembea kifua mbele kwani Miradi mingi iliyoibuliwa na wananchi kutoka kwenye Mitaa yao ikiwemo Afya, Umeme, Maji, Elimu, Miundombinu pamoja na shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi imetekelezwa kikamilifu na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naye Waziri wa Ujenzi Mhe, Abdallah Ulega alipata fursa ya kutoa Salama kwa wajumbe hao amewakikishia kuwa Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amenuia kwa dhati kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Tanzania kwa moyo wake wote wakiwemo wa Jimbo la Morogoro Mjini na ndio sababu Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutenga fedha kiasi cha Tsh. Bil. 50 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kihonda SGR pamoja na kurekebisha madaraja na Barabara zilizohariwa na Mvua
Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Morogoro Manispaa ndugu Twalib Berege amesisitiza kwa Mabalozi na Wenyeviti hao kuwa Chama hakitasita kuchuwa hatua za kinidhamu kwa kiongozi yoyotewa wa Mtaa ambaye atabainika kwamba hawatendei haki ya kuwatumikia wananchi waliompa dhamana kupitia CCM na hatua hiyo ni kumsimamisha uongozi kwa hatoshi kuwatumikia wananchi wa eneo husika