Mbunge wa Chama cha Conservative ambaye jina lake halijatajwa amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.
Polisi wa Metropolitan mjini London wameithibitisha kuwa mwanamume mmoja alikuwa kizuizini kwa tuhuma za alizofanya kati ya 2002 na 2009.
Shirika la Utangazaji la BBC limeripoti kuwa Chama cha Conservative kilisema kuwa aliombwa na kinara mkuu kutohudhuria Bunge wakati uchunguzi ukiendelea.
Mwanamume huyo pia anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya nafasi ya uaminifu na utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma.