Top Stories

Mbunge aliechaguliwa ZNZ kabla ya kuapishwa ajiuzulu

on

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimepokea kwa masikitiko barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mteule wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpeka Faki leo August 02, 2021.

“Katika barua ya Sheha ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kifamilia jambo ambalo Chama hakina uwezo wa kumzuia hasa ikizingatiwa kwamba ni haki yake ya msingi kama ilivyo kwa haki ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ndani ya CCM” ———Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Sheha Faki amejiuzulu siku chache tu baada ya kutangazwa Mbunge mpya na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili 18 Julai 2021.

LIVE : IG SIRRO “MBOWE AWE MKWELI SI ANASALI, USHAHIDI TUNAO”

Soma na hizi

Tupia Comments