Top Stories

Mbunge atoa Milioni 120 wapewe Wanafunzi ” Nawapenda sio sifa” (+video)

on

Mbunge wa Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, Haroon Primohamed ametekeleza ahadi aliyoahidi wakati wa Ziara ya Rais John Magufuli ya kuwashonea sare za shule wanafunzi wote wa darasa la saba watakaofauru na kujiunga kidato cha kwanza katika Wilaya hiyo.

Mbunge huyo ametekeleza ahadi hiyo kwa kukabidhi hundi ya mfano ya Sh. Milioni 120 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ambazo ni kwa ajili ya sare za wanafunzi 4800 wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza Januari mwakani.

Amesema kutokana na idadi ya wanafunzi waliofauru kila mwanafunzi atapata mgawo wa shilingi 25,000 ambazo zitawafikia kupitia kwa wakuu wa shule wanazotakiwa kujiunga nazo.

VIDEO HD: LIPUMBA AFUNGUKA RAIS MAGUFULI KUTUNUKIWA SHAHADA

Soma na hizi

Tupia Comments