Mbunge wa Jimbo la Segerea jijini Dar es salaam Bonnah Kamoli amefikisha kilio cha wamama wa jimbo hilo kuhusu urasimu unaotokea katika upatikanaji wa mikopo ya asilimia kumi ya wanawake,vijana,na walemavu kwani wengi wao wanao omba hukosa huku wakitakiwa kujaza fomu nyingi.
Akitoa kero hiyo katika mkutano wa wanawake wa jimbo la Segerea amesema kwasasa wanawake wanapata tabu kuendesha shughuli zao kwani wengi wao walitegemea mikopo hiyo ili biashara zao ndogo ndogo ziendelee lakini kusimamishwa kwa mikopo hiyo kumefanta wengi wao kuteseka kupata huku urasimu wa wasimamizi wa utoaji wa mikopo hiyo kuwaumiza zaidi wananchi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akijibu kilio hicho amesema kwasasa wameandaa utaratibu mpya wa utoaji mikopo hiyo na kwasasa wanadai zaidi ya bilioni 21 ambazo bado zipo kwa wananchi hawajarudisha .
Ameongeza kuwa utaratibu mpya utakao kuja hautakua tena na vikundi hewa au watu ambao hawafahamiki kupata mikopo na kuwataka wanawake kuchangamkia fursa ya mikopo itakapoanza tena kwa kuwa na utayari.