Mbunge wa Viti Maalum Vijana CCM, Mariam Ditopile amekabidhi msaada wa vitanda na magodoro 24 yenye thamani ya Milioni 6 katika Shule ya Msingi Bereko wilayani Kondoa, Dodoma ambayo ina kitengo cha Watoto wenye mahitaji maalum.
” Msaada huu nimeutoa kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kuwapatia watoto wetu elimu bila malipo, hivyo niwasihi wazazi wenye watoto wenye Ulemavu kuwapeleka shule watoto hao ili waweze kupata elimu kama wenzao na kuweza kufanikisha ndoto zao,” Ditopile.