Mbunge wa jimbo la Gairo Shabiby amesema kuwa kukamilika kwa shule mpya ya Sekondari Amali kutaleta tija ya kukuza maendeleo kwenye sekta elimu ya katika Kata hiyo
Akizungumza katika mkutano maalumu wa uzinduzi wa utekelezaji wa miradi jimboni humo amesema kuwa zaidi ya Bilioni moja na milioni 600 (Bil 1.6) zimetolewa ili kuhakikisha shule hiyo inakamilika yenye kuanzia kidato Cha kwanza hadi Cha sita
Shabiby amewaomba wananchi kuwa na ushirikiano katika ujenzi wa shule hiyo na kuwa wazalendo katika kutunza na kulinda miradi yote iliyomo ndani ya jimbo la Gairo
Katika uzinduzi huu Mhe. Shabiby pia amesema kuwa ujenzi wa madaraja mawili makubwa ambayo hapo awali yalionekana kuwa ugumu wa kukamilika hivi sasa mkandarasi ameshaanza kazi na hivi punde madaraja haya yatakamilika
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Gairo Sharifa Nabalang’anya amesema kuwa katika uzinduzi kilichobaki na usafishaji wa mazingira kwani tayali kiasi Cha fedha ambazo ni zaidi ya ya Bilioni moja na milioni 600 tayali zimewekwa katika akaunti ya shule
Nao baadhi ya wananchi wamesema kuwa hapo awali wanafunzi walikuwa wakisafiri eneo la umbali mrefu kwa ajili ya kwenda shule kukamilika ujenzi wa shule hiyo kutasaidia wanafunzi kusoma Kwa wakati.