Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/22.
“Asilimia 50 ya presha ambayo watu wanayo sasa hivi ni suala la elimu na suala hili sio kwenye elimu yenyewe, leo nimekuja na mfano wa daftari ambazo shule zinasomea, shule binafsi wanasomea daftari la sh 200 ambapo kwa mwanafunzi madaftari 11 itakuwa 2200 lakini shule ya Serikali inasomea counter book, counterbook 11 ni sawa na sh 55,000 ambayo ni sawa na gunia la mahindi au mpunga” Mbunge Kishimba
“Sasa inawezekanaje matajiri wakasomea daftari la Sh 200, maskini wakasomea daftari la sh 5500 na mnasema watu wana stress ni kweli watu hawana raha na shule, nina mfano wa uniform hapa, shule za binafsi ni rangi hizi, uniform za shule za Serikali ni rangi nyeupe ni vipi mzazi ataweza kufua kila siku, Wazazi wanashinda wananunua sabuni na kufua tunaongeza umaskini badala kuongeza elimu”-Mbunge Kishimba