Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga ametoa msaada wa bati 80 na fedha taslimu Shilingi Milioni Moja kwa Shule ya Sekondari Muhwana iliyopo katika Halmshauri ya wilaya ya Iringa kama miongoni mwa juhudi zake binafsi kuunga mkono Serikali ya awamu ya 6 kuboresha miundombinu mbalimbali ya elimu shuleni hapo na hamiyae kukuza hali ya kufundishia na kujifunza.
Mbunge Kiswaga ametoa msaada hu leo wakati wa muendelezo wa ziara yake Jimboni humo.
Amesema msaada huo utakwenda kuwa chachu ya kuongeza hali ya ufundishaji kwa walimu na kujifunza kwa wanafunzi.
Akishukuru kwa niaba ya uongozi wa Shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Muhwana, Donald Kilundo amesema msaada huo umekuja wakati muafaka na kuahidi kuutumia vizuri kwa malengo kusudiwa.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Magulilwa, Vitalis Samila amesema Mbunge Jackson Kiswaga amekuwa na mchango mkubwa kwenye kusukuma maendeleo