Mbunge wa Viti Maalum Lucy Mayenga ameiomba Serikali kupitia Wizara Maji kupeleka huduma ya maji katika maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga ambapo kuna baadhi ya wilaya mpaka leo zimekuwa zikisumbuliwa na changamoto ya ukosefu wa maji.
Akizungumza wakati akichangia bungeni jijini Dodoma Mhe. Lucy Mayenga amesema kuwa “Inauma sana mradi wa ziwa Victoria unapita lakini hakuna huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo yale hivyo Serikali itusaidie sana maji kwa wakazi wa wilaya ya Kishapu”
Mbali na hayo Mhe Lucy amegusia pia suala la upatikanaji wa bidhaa ya sukari ambapo amepongeza hatua zilizochukuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kupambana na changamoto ya uhaba wa bidhaa hiyo.
“Rais Samia ndiye kiongozi pekee aliyejitokeza hadharani na kupambana na suala la sukari, amefanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na ameonyesha uzalendo usiokuwa na mashaka” ameongeza Mhe. Mayenga