Mbunge wa Makete, Festo Sanga amependekeza Serikali kuweka viwango vya mishahara ya Wachezaji wa mpira wa miguu Tanzania kwa madai kuwa wanafanya kazi kubwa na nzuri lakini malipo wanayopata ni kidogo sana.
Sanga ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
“Wachezaji wetu wanachangamoto ya maslahi, ni wakati sasa tuweke kiwango cha mishahara, wanacheza kwa jasho na damu wanalipwa Tsh 200,000, ikitokea wakilazwa hospitalini tunaanza kuchangishana, lazima tuweke kiwango mchezaji wa ligi kuu lazima alipwe Milioni 1 kwenda juu”
Baadhi ya nchi za Afrika kama Cameroon tayari wameanza kufanyia kazi suala la kiwango cha mishahara kwa wachezaji FCFA 100,000 ambapo ni zaidi ya Tsh 379,591, hiyo ikiwa ni miezi michache tu baada ya mchezaji wa zamanı wa Cameroon, FC Barcelona, Inter Milan na Chelsea Samuel Eto’o kushinda Urais wa shirikisho la soka Cameroon (FECAFOOT).
HAJI MANARA ATANGAZA KUMTAFUTA AHMED ALLY WA SIMBA “DOGO ANA MBINU ZAKE ZA KISASA”