Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amedai kuwa suala la mfumuko wa bei nchini limesababishwa na usimamizi dhaifu wa sheria na usimamizi dhaifu wa sera za fedha licha ya kuzitambua sababu nyingine za Vita ya Ukraine na Covid 19 ambazo zimekuwa zikitajwa sana.
Mpina ametoa hoja hiyo leo Bungeni February 1, 2023 wakati akichangia mjadala wa kuhusu taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2022 pamoja na taarifa ya Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
“Huwezi ukacontrol mfumuko wa bei kama usimamizi wako wa bajeti hauko sawasawa, Tsh. Bilioni 350 tumemlipa Symbion, fedha ambazo hazipo kwenye bajeti lakini pia kama huwezi kupeleka fedha zilizopangwa kwenye maeneo husika hasa kwenye sekta muhimu kama kilimo, jana tumeambiwa mpaka February, 17% ya fedha ndizo zilizopelekwa, utacontrol vipi mfumuko wa bei?”