Bunge limepitisha kwa pamoja makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Madini kiasi cha shilingi bilioni 83,445,260,000.0 kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kwa mchanganuo wa Shilingi 22,000,000,000.0 ikiwa ni fedha za maendeleo,Shilingi 61,445,260,000.0 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Kati ya fedha hizo, shilingi 20,609,600,000 ni kwa ajili ya Mishahara na shilingi 40,835,660,000.0 ni Matumizi Mengineyo.