Mbunge wa Israel aliyeunga mkono mswada ambao ungezuia shirika kuu la Umoja wa Mataifa huko Gaza na Ukingo wa Magharibi kufaMbungenya kazi nchini Israel amemshutumu balozi wa Marekani nchini Israel kwa kuwashawishi viongozi wa upinzani kuzuia hatua hiyo.
Ikiwa mswada huo utapitishwa katika bunge la Israel, Knesset, wiki hii, itakataza afisa yeyote wa Israel kutoa huduma au kushughulika na wafanyakazi wa Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa na kukataza UNRWA kufanya kazi nchini Israel.
Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marekani, zimeelezea wasiwasi wake juu ya athari za mswada huo.
Serikali ya Israel imedai kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi (UNRWA) wana uhusiano na Hamas. UNRWA imekanusha vikali madai hayo, lakini serikali kadhaa zilisitisha ufadhili wa shirika hilo mapema mwaka huu huku madai hayo yakichunguzwa.
Mbunge huyo, Yulia Malinovsky, aliiambia CNN kwamba Balozi wa Marekani Jacob Lew amewasiliana na viongozi kadhaa wa upinzani, akiwemo Avigdor Lieberman, Yair Lapid na Benny Gantz, katika juhudi za kusimamisha sheria hiyo.
Alielezea shinikizo la Marekani kama lisilokubalika.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliiambia CNN kwamba kama suala la kisera, haitazungumzia mazungumzo ya kibinafsi ya kidiplomasia.
Lakini ilisema kwamba sheria iliyopendekezwa itafanya kuwa haiwezekani kwa UNRWA kufanya kazi na itaacha “tupu ambayo Israeli itawajibika kulijaza.” Msemaji alisema UNRWA ilitoa huduma muhimu huko Gaza, Ukingo wa Magharibi, Lebanon na Jordan.
UNRWA imekuwa ikilengwa kwa muda mrefu na upinzani wa Israel na uhusiano kati ya Israel na Umoja wa Mataifa umedorora kutokana na vita huko Gaza.