Sekta ya madini ni Moja ya Sekta muhimu nchini ambayo inachangia Kwa kiasi kikubwa Pato la Taifa ambapo wawekezaji wazawa na kutoka nje ya nchi wameendelea kuwekeza Ili kuhakikisha inawanufaisha mwanachi Mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.
Katika kuendelea kuhakikisha sekta hiyo inakua Kwa Kasi nchini mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham ambaye m Mkurugenzi wa kampuni ya Rubby International amefungua tawi la ofisi ya ununuzi na uuzaji wa madini ya Vito katika nchi Thailand jiji la Bangkok ikiwa ni jitihada ya kutangaza fursa zilizopo nchini tanzania kupitia sekta muhimu ya madini.
Salim anasema kufungua kwa tawi hilo kutaleta chachu ya kuitangaza nchi ya tanzania kupitia madini hii ni kutokana na umuhimu wake pamoja na kuvutia Watalii kupitia sekta hiyo.