Balozi wa Utalii wa Tanzania, Nangasu Warema leo Februari 10,2023 ametoa maoni yake kuhusu mwelekeo wa uchumi kutokana na mjadala ulioibuka bungeni mwanzoni mwa wiki hii.
Balozi huyo wa utalii amesema kwamba mataifa mengi duniani yameathirika kiuchumi ikiwamo Tanzania ambayo tayari hatua madhubuti zimechukuliwa.
Amesema miongoni mwa hatua ambazo Tanzania imechukua ni pamoja na Rais Samia kutoa ruzuku kwenye mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa karibu Sh100 bilioni kila mwezi.
Warema amesema eneo jingine ambalo Serikali ya awamu ya sita imetoa ruzuku ni kwenye bei ya mbolea na mbegu ili kuwarahisishia wakulima upatikanaji wake kwa urahisi.
Amesema kitendo cha Rais Samia kuamua kuongeza bajeti ya kilimo mara nne zaidi ya mara ya kwanza, kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji vitaongeza kilimo cha tija kwa watanzania.
“Sasa hivi Tanzania ndiyo kimbilio la chakula kwa nchi zote za Afrika Mashariki na kati,” imeeleza sehemu ya taarifa ya balozi huyo