Michezo

Sharti walilopewa Mbuyu Twite na Kavumbagu ikiwa wanataka kuendelea kuicheza Yanga

on

Screen Shot 2014-03-22 at 12.27.42 PMMbuyu Twite na Didier Kavumbagu wa Yanga wana siku 30 tu za kuitumikia klabu hiyo kabla ya kufanya uamuzi mgumu wa kubaki au kuondoka Yanga ambapo siku hizo zinaanza leo mpaka Aprili 19 msimu utakapomalizika na Aprili 20 watakuwa na kikao Jangwani kutathmini msimu ikiwemo kupongezana kama watafanikiwa kutetea ubingwa wao.

Mastaa hao ni miongoni mwa wachezaji nane wa Simba na Yanga ambao wapo sokoni na wanaweza kusaini mkataba na klabu yoyote muda wowote kuanzia sasa na siku ambazo klabu zao zitawamiliki kihalali hazizidi 30 kuanzia sasa.

Ingawa klabu zao zimekuwa bize kuwania nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, baadhi ya wachezaji hao wameanza nyodo na kusisitiza kwamba hawatasaini na klabu hizo mpaka mwisho wa msimu huku ikionekana kama wanataka kutingisha kiberiti wapewe dau nono.
KAVUMBANGUUchunguzi wa Mwanaspoti ambao umethibitishwa na wachezaji hao umeonyesha kwamba wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwezi Aprili 19 Ligi ya Bara itakapomalizika ni kipa, Ali Mustapha ‘Barthez’ ambaye habari za uhakika zinaeleza mazungumzo yake ya kurejea Simba yanakwenda vizuri, beki wa pembeni Mbuyu Twite, washambuliaji Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi aliyegoma kutolewa kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Kwa upande wa Simba wachezaji wanne ambao mikataba yao ipo ukingoni ni viungo, Uhuru Selemani na Ramadhani Chombo ‘Redondo’, kipa raia wa Ghana Yaw Berko ambao wote hata hivyo hawajawahi kuwa na uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.Mchezaji mwingine ni beki wa pembeni Haruna Shamte.

Twite amesisitiza kwamba hatosaini mkataba mpya na Yanga mpaka msimu utakapomalizika huku ikitafsiriwa kwamba anataka kutingisha kiberiti ili kurekebishiwa baadhi ya vipengele kwenye mkataba wake na amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba hana raha kwa jinsi anavyoishi na vigogo wa Yanga kwa sasa.

Habari za ndani zinadai kwamba mchezaji huyo amewahi kufanya mazungumzo na viongozi wa Azam miezi michache iliyopita hivyo ana imani kwamba huenda wakampa ofa.

Kavumbagu ambaye amekuwa tegemeo kwenye fowadi ya Yanga alisema: “Bado sijasaini mkataba mwingine wa kuichezea Yanga, mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu huu (Aprili 19), ingawa tayari nimeanza mazungumzo ya awali ambayo bado hatujafikia muafaka wa kusaini mkataba mpya.”

SOURCE: GAZETI LA MWANASPOTI

Tupia Comments