Leo March 55, 2018 moja ya stori inayoshika headlines ni kuhusu kulazwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) AyoTV na millardayo.com imezungumza na Afisa uhusiano wa hospitali ya rufaa ya KCMC Gabriel Chisseo.
Chisseo amesema Freeman Mbowe amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa anaumwa kichwa na sababu za kitabibu zinaeleza ni kutokoana na uchovu.
Ameongeza kuwa amewekwa kwenye wodi maalumu na Madaktari wameshauri apumzike huku hali yake ikiwa inaendelea kuimarika.
“Yupo hapa kwetu Madaktari wetu wanaendelea kumhudumia kwa ukaribu zaidi na anaendelea vizuri, Madaktari wetu watafanya vipimo vingine nadhani baadae tutatoa majibu” -Gabriel Chisseo
TAARIFA RASMI YA CHADEMA KUHUSU KULAZWA KWA MBOWE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
MAHAKAMA YA RUFAA DHAMANA YA RUGEMARILA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA