Kijana Frank Patrick (Mchekeshaji wa Mtandaoni ) Maarufu Kama Molingo (17) Mkazi wa wilaya ya Chato , Mkoani Geita amefariki Dunia usiku huu akiwa nyumbani kwao Chato ambako alikuwa akiuuguzwa na Mama yake Mzazi.
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kwa Rafiki ake ambaye alikuwa akiishi naye Mudi Msomali anasema Molingo alikuwa anaugua mara kwa mara na chanzo cha ugonjwa Bado hakijajulikana huku wakisema alikuwa muda mwingine anavimba mwili na kuishiwa Damu Mwilini.
” Molingo bwana alikuwa anaumwa maradhi hayaeleweki kila wanachopima hawaoni kitu kwahiyo ndio hivyo mara ya kwanza walihisi labda ni sikoseli walipima akawa yuko sawa wakawa wanahisi bandama mara moyo yaani kiufupi anarudi kwao hatukujua shida hasa ni nini , ” Rafiki wa Molingo , Mudi Msomali.
” Madaktari walishauri mpelekeni kwao kwahiyo nahisi walikuwa wameshaona ila mimi tu kama mtu mzima nilijiongeza nikamwambia Anna itakuwa labda wameona mbali wanashauri mmurudishe kwao kwahiyo ndio hivyo alikuwa anavimba tuu mwili anaishiwa Damu mara kwa mara , ” Rafiki ake Molingo , Mudi Msomali.