Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi amekamatwa na Polisi akiwa na Waandamanaji wengine nje ya Majengo ya Bunge la Kenya ambako wameandamana leo wakilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa ikiwemo vyakula kunakosababisha ugumu wa maisha kwa Wananchi.
Polisi wamefyatua mabomu ya machozi kuwatawanya Waandamanaji hao huku wengine wakikamatwa wakiwemo Wanaume mbalimbali waliokuwa vifua wazi wakiongozwa na Omondi.